BALOZI WA KOREA YA KUSINI NCHINI TANZANIA AITEMBELEA WILAYA ILEMELA
Safari ya kuijenga Ilemela mpya inazidi kuchanja mbuga ambapo Siku ya
jana Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Mhe Song Geum Young amezuru
Manispaa Ilemela na kutembelea Kijiji cha Ihalalo kilichopo kata ya
Sangabuye eneo linalotarajiwa kujengwa kijiji cha maendeleo mfano wa
Semau Dong nchini Korea
Akizungumza baada ya kuwasili Kijijini hapo Mhe Song amesema kuwa
ametembelea kijiji cha Ihalalo kufahamu vizuri eneo litalojengwa kijiji
cha mfano ili kuwarahisishia wananchi Kupata huduma muhimu katika
kujieletea maendeleo
'… Mhe Rais wenu wa awamu ya kwanza alihimiza juu ya Uhuru na kazi na
huyu wa Sasa anahimiza kufanya kazi, Sisi tutaendelea kushirikiana na
Serikali yenu katika shughuli za maendeleo…'
Mhe Song pia ameahidi wananchi hao juu ya ujio wa wataalamu wa umeme wa jua watakao wasili kijijini hapo mapema mwakani
Nae mkuu wa wilaya Ilemela Dkt Leonard Masale aliyeambatana na Mstahiki
Meya wa Ilemela Mhe Renatus Mulunga wamemuhakikishia balozi huyo juu
utayari wa wananchi na Serikali katika kuwatumikia wananchi hao
'… Sisi kazi yetu ni kuwatumikia wananchi hivyo tunawakikishia utayari
wa wananchi hawa na Serikali yao…' alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya
Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameendelea na Ziara
yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo ambapo siku
ya jana alikuwa kata ya Nyasaka
Mhe Mbunge amewasisitiza wananchi wa kata hiyo juu ya kuitumia fursa ya
urasimishaji wa makazi na kuwataka wamiliki wa viwanja visivyoendelezwa
kuviendeleza mara moja
'… Urasimishaji maanake ni kwamba kasi ya ujenzi ilikuwa ni kubwa kuliko
upimaji kwasababu serikali yenu ni sikivu badala ya kiwabomolea ikaamua
kuwarasimishia…' amesema Mbunge huyo
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyasaka na Naibu Meya wa Manispaa
Ilemela Mhe Shaban Maganga amemshukuru Mhe Mbunge kwa ziara zake
anazozifanya Jimboni na kumhakikishia ushirikiano katika kuwaletea
wananchi maendeleo
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
21.12.2016
No comments:
Post a Comment