Aliko Dangote alizaliwa
tarehe 10-04-1957
huko Kano Nigeria, Dangote ni raia wa Nigeria tangu 1957 hadi sasa.
Dangote anatoka katika familia ya kiislamu yenye utajiri mkubwa unaotokana na biashara. Dangote ni mjukuu mkubwa wa kiume wa mzee Alhaji Alhassan Dantata mwafrika aliyekuwa tajiri hadi alipofariki mwaka 1955. Baada ya miaka miwili ya kifo cha babu yake, Dangote alizaliwa na baada ya kutimiza umri wa kwenda shule alikwenda kama watanzania wanavyofanya wanapofikia umri wa kwenda shule, alifanikiwa kusoma masomo ya biashara katika chuo kimoja jijini Cairo, Misri, chuo hicho kinaitwa Al-Azhar University. Dangote alikaririwa akisema alipenda sana kuwa mfanyabiashara tangu akiwa mdogo sana kwani alipenda kuuza pipi hali ambayo ilimsukuma kuipenda shughuli hiyo na ndiyo imemfikisha hapa alipo kwa sasa. Dangote anashikiria namba moja kwa utajiri barani Africa na pia ni mtu wa 30 duniani kuwa tajiri kwa takimwu za mwaka 2013.

ALIKO DANGOTE |
Mnamo mwaka 1977,
Dangote akiwa na miaka 20 tu alisajili kampuni ndogo iliyokuwa ikijihusisha na
biashara ndogondogo yaani small trading firm, hivi sasa kampuni hiyo imekuwa
kubwa kiasi cha kuteka soko la Africa kwa uzalishaji wa sukari kwa ajili ya
viwanda vya kutengeneza vinywaji laini,
bear, nk. Dngote hivi sasa amewekeza katika mataifa mbalimbali kama Benin,
Togo, Nigeria, Ghana, Tanzania, Kenya na Ethiopia. Kazi yake kubwa barani Africa ni kuzalisha na
kusambaza cement, sukari, unga, na uchukuzi wa mizigo(freight). Nchini Nigeria Dangote
group linaongoza kwa usambazaji wa sukari viwandani kwa ajili ya vinywaji
laini, bia, na bidhaa tamutamun(confections). Hivi sasa kampuni yake si kampuni
ya biashara ndogondogo, bali ni mkusanyiko wa viwanda vikubwa nchini Nigeria ikijumuisha
1. Dangote Sugar
refinery
2. Dangote cement
3. Dangote Flour
Hivi sasa dangote
anamiliki soko la sukari kwa zaidi ya 70% ya soko zima. Dangote anaongoza kwa
kuwa na viwanda vya kusafisha sukari barani Africa na cha tatu duniani, sasa
unaweza kuona ni kwa namna gani jamaa amejipanda kushindana kidunia na si kwa Africa
tu. Dangote huzalisha tani 800, 000 za sukari kwa mwaka. Vipo vitu vingi
vinavyomhusu jamaa, nimekuletea vichache tu.
CHA
KUJIFUNZA
Dangote nilipokuwa
sijamwona kwa macho yangu nilikuwa najua kuwa ni mtu mnene mwenye kitambi na
mtu mwenye kujikuza sana kulingana na utajiri alionao lakini baada ya juzi
kumwona pale Ikulu akiongea na rais Magufuli nilishangaa sana, katika maisha ya
kawaida na namna tunavyoshuhudia hapa Tanzania kwa wenye pesa, ni shida sana. Leo
hii mtu anamiliki Paso tu tena used lakini anataka kupasuka, hivi ikitokea huyo
mtu akapat pesa kama za Dangote jamii itajifunza nini kutoka kwake? Tunapaswa kusimama
kidete bila kukata tama, ukiweka nia katika jambo Fulani ni lazima utatoka tu. Kupitia
Dangote tunajifunza kwamba, tujitahidi kwa vyovyote vile tuwe wajasiriamali ili
na sisi tuwaajiri watu ili kuongeza nguvu kwenye soko la ajira, haiwezekani
tuwe tunakaa tu na kusubiri mishahara bila kuwaza tufanye nini ili tupate pesa
zitakazotufanya na sisi tuwekeze na hatimaye kuiona Tanzania mpya ambayo vijana
wanaotoka vyuoni na kuhangaika kutafuta ajira wasihangaike tena. Akili ni pesa
tosha za kutuwezesha kuwekeza ila bado tunasita sit sana kuanza mara moja na
kuwa wavumilivu kwa changamoto zitakazokuwa zinatunyemelea katika kutimiza
malengo.
Makala hii imeandaliwa
na mimi
John Mgejwa
0759708499
No comments:
Post a Comment