Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Sunday, 11 December 2016

Dhana potofu katika jamii kuhusu ualimu

Matokeo ya kidato cha nne yanapotoka utasikia kauli hii "mtoto wa fulani amefeli sana", baada ya hapo utamsikia mwingine wa pembeni akishangaa " hata ualimu hapati duh basi amefeli". Hivi ni nani amewaloga? Ni nani aliwaambia kwenda ualimu ni mteremko? Mawazo haya mnayatoa sayari gani hiyo? Utakuta anayezungumza maneno hayo hata shule hajakwenda ingawa kuna wasomi pia wenye mawazo hayo ambao walisha kata tamaa ya maisha wanasoma kutafuta ‘title’ mtaani. Fuatilieni kwa makini katika taifa hili utagundua kuwa ngazi ya cheti-nursing inasomwa na watu wengi ambao wana matokeo mabaya kuliko ualimu wa shule ya msingi maana wakati ule daraja la 4 lilianzia 26-33 lakini katika hizo points ualimu mtu aliingia kwa points 26-28 tu lakini kwa nursing walichukuliwa hadi points 30 ilimradi awe na D katika biology, chemistry, na Physics. Lakini bado wanafanya vizuri katika hiyo fani. na kuna watu tunawajua waliingia nursing na 31, 30 nk. Mbali na nursing zifuatazo ni kada ambazo wengi wanaingia wakiwa na matokeo ya kuchechemea kuliko ualimu (i) astashahada ya uandishi wa habari (ii) astashahada ya maendeleo ya jamii (iii) astashahada ya procurement (iv) astashahada ya sheria (v) astashahada ya nursing (vi) astashahada ya uhasibu (vii) astashahada ya serikali za mitaa (viii) astashahada ya mipango vijijini, zipo nyingi sana ngoja niishie hizo. Tusichukulie ualimu kama ujinga bali taaluma iliyo na heshima kubwa. leo hii hata digrii za elimu baadhi ya watu wanazidharau eti ni rahisi, sasa ili kuondoa dukuduku lako hilo jiunge digrii ya education uone watu wanavyosota, kuna msuli wa kufa mbwa kwa yule aliyeenda kusoma na kutafuta maarifa ila huwa inaitwa digrii rahisi kwa watu waliokwenda kula chips chuoni na kusaka "c" .Taaluma zote ni ngumu na zinahitaji uelewa mkubwa wa mambo maana usipokuwa makini utatoka chuoni ukiwa " pumbalized" usisome kwa ku-’under evaluate’ digrii za wenzako tofauti na hapo utakuwa unasoma kutafuta "title tu" na ukirudi mtaani utakuwa hutofautiani sana na uliyemwacha mtaani wakati unakwenda chuo labda utakuwa umemzidi tu kwa kutafuna boom na kutetemeka maini wakati wa presentations za darasani. Akili ni mali lakini zikitumiwa vibaya huwa ni adui mkubwa wa kuleta maendeleo binafsi, ya familia na taifa kwa ujumla. Aliyeingia chuo kikuu kwa kupitia vyuo vidogo sababu ya matokeo mabaya ya kidato cha nne usimbeze hata siku moja mara nyingi hawa ndo huwa wanafika mbali kuliko hata yule aliyefaulu moja kwa moja hadi chuo kikuu. Jamii inapaswa kufundishwa katika hili tofauti na hapo basi ni dhahiri kuwa wasomi hasa walimu wataendelea kudharauliwa pamoja na kwamba wanaisaidia jamii kuondokana na ujinga.

Kama wewe ni mwalimu wa digrii unafundisha lakini bado unaona kama taaluma ya ualimu uliisoma kwa sababu ya kupata mkopo na kwamba nyumbani kwenu ni masikini na ualimu ulikuwa huupendi yaani bora ukaachia ngazi ili wale wanaoipenda taaluma yao waendelee kuchapa kazi, wewe ukiwa kama mwalimu ukipitiwa na maneno ya watu mitaani kwamba ualimu siyo taaluma nzuri bali ni ya watu waliofeli basi ujue elimu haijakusaidia, ukiwa mtu msomi tena mwenye digrii ukishindwa kujieleza kwa watu kama hao basi ujue wewe binafsi ulifeli na siyo watu waliosoma taaluma ya ualimu. Mtu uliyesoma hadi ngazi ya digrii unashindwaje kueleza kwa namna gani ualimu na walimu siyo taaluma ya watu waliofeli?

 Mwandishi wa makala hii ni John Mgejwa 0759708499

No comments:

Post a Comment