Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Thursday, 9 November 2017

MACHACHE KUHUSU POPO




Kuna zaidi ya aina (pecies)  1,100 ya Popo ambayo ni sawa na 25% ya mamalia wote walioko duniani


Popo ndio mnyama pekee anayeweza kuruka (fly) kama ndege, mara nyingi anatembea usiku, na huwa anakula wadudu wadodo wadogo, watu wengi wanadhani kuwa popo haoni kwa macho ila ukweli ni kwamba anaona vizuri kushinda hata wanyama wanaotembea mchana.

Popo anawezaje kuwakamata wadudu usiku? hii ni changamoto, ila popo amejitengenezea aina ya mawimbi ya sauti yanayomsaidia kuwinda, njia hii inaitwa echolocation. Hii inafanyeje kazi, kama ulishawai kutoa sauti kubwa kwenye pango huwa sauti inakurudia, vivyo hivyo na popo ndivyo inavyokuwa.

Popo ndiye mnyama pekee anayetoa hii sound waves duniani, cha ajabu ni kuwa hii sound wave inayotolewa na popo ni kubwa sana kushinda sauti zote hapa duniani na ipo nje wa uwezo wa binadamu kuweza kusikia, hapa ina maana ukisikia unaweza kuwa kiziwi au ukafa kabisa, hii sauti ikigonga kitu kiwe mti au mdudu inarudisha taarifa kwenye ubongo wake na kutafsiri na popo anakuwa tayari amejua ni kitu gani hicho na kipo umbali gani

Ukipima frequency ya sound waves ya popo ni makadirio kuanzia 14,000 mpaka 100,000HZ ambapo binadamu ana uwezo wa kusikia kuanzia 20 mpaka 20,000HZ. Tofauti ni kubwa sana.

Profesa Hughes anasema hivi: “Hebu wazia mfumo wa kupokea mwangwi ulio tata kuliko ule wa nyambizi ya hali ya juu zaidi. Sasa wazia mfumo huo ukitumiwa na popo mdogo sana anayeweza kutoshea katika kiganja cha mkono wako. Ubongo wake ambao ni mdogo kuliko ukucha wa kidole gumba humwezesha kutambua umbali, mwendo, na hata aina ya wadudu anaonuia kukamata!”

Mbali na popo, kuna angalau aina mbili za ndege wanaotumia mwangwi kutambua mahali vitu vilipo. Ndege hao ni mbayuwayu fulani wa Asia na Australia na ndege aina ya oilbird wa Amerika Kusini. Hata hivyo, inaonekana ndege hao hutumia uwezo huo kuwasaidia tu kusafiri katika mapango yao yenye giza.

Black Winged Bat yeye ni insectivore yaani anakula wadudu wadogowadogo na saizi ya kati, Popo huyu mmoja anaweza kula hadi mbu 1,200 kwa saa moja.


No comments:

Post a Comment