Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Thursday, 9 November 2017

Prof. Tibaijuka, 2020 nitwaachia vijana wagombee



Mbunge wa  Muleba Kusini (CCM), Prof Anna Tibaijuka, ametangaza kung’atuka nafasi ya ubunge kwa kutogombea tena kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.


Prof. Tibaijuka alitangaza msimamo huo jana mkoani Kagera, wakati wakizungumzia miaka miwili ya serikali ya Rais John Magufuli ambaye hivi sasa yuko  mkoani humo kwa ziara za kikazi.

Jumatatu ya wiki iliyopita, Lazaro Nyalandu, ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), alitangaza kujiuzulu ubunge na pia kujivua uanachama wa CCM kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho.

Baadaye Nyalandu alionekana akikaribishwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Kisheria, kuhama chama humpotezei mbunge sifa ya kuendelea kuwa mwakilishi wa jimbo lake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huandaa uchaguzi mwingine mdogo kwa ajili ya kumpata mbunge mwingine kwenyejimbo husika.

Wakati akifafanua kuhusu uamuzi wake wa kugombea tena ubunge mwaka 2020, Tibaijuka aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, aliliambia Televisheni ya Taifa (TBC), kuwa ameamua kujing’atua ili kutoa nafasi kwa vijana.

“Sisi ni watu wazima…. Kizazi chetu tumeshamaliza kazi. Tumeshasitaafu na mimi nikimaliza ubunge muhula huu nastaafu, nakwenda Muleba,” alisema Tibaijuka na kuongeza: “Na kuaga nimeshaaga na wananchi wameniamini. Napenda tuwape nafasi vijana. Kuzeeka haimaanishi kwamba maarifa yangu yaondoke kwa sababu nimestaafu, tunawapa nafasi vijana washike nchi.

No comments:

Post a Comment