Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Wednesday, 10 February 2016

DUNIA YETU HAIJATULIA

"Kijiografia, dunia yetu haiko salama, ndani ya uso wa dunia kuna nguvu kubwa inayofanya kazi kuliko tufikiriavyo. Hebu fikiria namna ambavyo mlipuko wa kivolkano hutokea, kwa maana hii ya ndani ya uso wa dunia kuwa na nguvu kubwa zinazofanya kazi kuzidi mashini tuzijuazo hapa juu ya uso wa dunia, ni dhahiri kuwa hapo ulipo wakati huu unaweza kushtukia ardhi ikazama ndani. Ndani ya uso wa dunia kuna mashimo pia, hivyo mkwanguo wowote haijarishi ni wa maji au upepo juu ya ardhi unaweza kusababisha yale mashimo kuwa karibu zaidi na hapo ulipoketi juu ya ardhi. Popote ulipo hauko salama, dunia haijatulia, usije kushangaa siku moja tetemeko la ardhi likapita kwenye ziwa kubwa kama victoria, nk na hii inaweza kusababisha maafa makubwa kwani mawimbi yataongezeka kwa ukubwa na nguvu na kusababisha yawe na nguvu kubwa kama tunavyosikia kila kukicha huko Japani. Sisi hatuko kwenye huo ukanda wa matetemeko lakini ni vizuri kuchukua tahadhari ya kujikabithi kila siku kwa Mungu, bila kujali ni usiku kiasi gani, ni jua kali kiasi gani na umechoka kiasi gani kumwomba Mungu wetu.Wanajiografia hutumia sana nadharia ya isostasia inayosema kuwa " dunia hujiweka yenyewe katika hali ya usawa kutokana na mambo mbalimbali ya asili yanayotokea juu ya uso wa dunia na kwamba watu hawawezi kutishwa na hizo nguvu za ndani kwa ndani maana kuna nguvu zingine za asili ambao zinaweza kuzuia madhara endapo yatatokea, hivyo yatadhibitiwa kabla ya kutokea. Ni jambo jema lakini leo hii ukiwaambia watu wa Japani kuwa isostasia inasema hivyo, watakushangaa maana hadi leo hii wanasumbuliwa na matetemeko ya ardhi yanayotokea ndani ya bahari na kusababisha tsunami zisizo na kikomo. Ndiyo maana nasema kila wakati yatupasa kumwomba Mungu, hii ikiwa na maana kuwa hujui lini na wapi hizo nguvu za ndani ya uso wa dunia zitatetemesha dunia na kujikuta umedumbukia ndani, au ukashtukia ardhi ikakumeza.

No comments:

Post a Comment