Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Saturday, 13 February 2016

MIMI NA WEWE NDIYO WAKOMBOZI WA TAIFA HILI LA TANZANIA

Kwa muda mrefu watanzania walipoteza matumaini na taifa lao, hii ni kutokana na miiko ya uongozi kukiukwa kwa asilimia kubwa na watendaji wakuu wa serikali, ikulu kupoteza mvuto wake ambao ilikuwa nao miaka 1960. Hali hii pia ilifikia hadi watanzania wenyewe kupoteza roho ya kizalendo kutokana na kwamba ilifikia hatua nchi ikawa kama haina viongozi wa juu katika serikali hivyo na kujikuta kana kwamba wanajiongoza. Mara nyingi mtu anapohisi anajiongoza ni dhairi kwamba hufanya mambo yake kwa kujiamlia na ndiyo maana watanzania waliweza kufanya mambo watakavyo, amhudumie mtanzania mwenzake au asimhudumie yote yalikuwa sawa. Hata kule mashambani au katika biashara mtu alikuwa akifanya kana kwamba shamba au biashara siyo yake na ndiyo maana maisha yetu yaliendelea kuwa hivi tulivyo. Ni jambo jema kwamba angalau hii kashikashi tunaoushuhudia katika taifa hili sasa watu wanabadilika kikogo katika utendaji kazi, ingawa sijui kama watu wasio katika taasisi za binafsi wanajituma kufanya kazi kwa bidii ili kumpa moyo wa uzalendo zaidi mkuu wa nchi yetu. Kitendo cha watu kufanya kazi kwa mazoea kisishughulikiwe katika taasisi za umma pekee, waajiri katika taasisi za binafsi pia wawakazanie wafanyakazi wao wafanye kazi kwa nguvu zote ili taifa lisonge mbele. Ni juzi juzi tu waziri wa fedha na mipango mheshimiwa Mpango aliuambia umma kuwa 'Udhibiti wa safari zisizo za lazima nje ya nchi miongoni mwa maofisa wa serikali umewezesha kuokolewa kwa zaidi ya Tshs. 20 bilioni katika miezi mitatu iliyopita.' Hii inadhihirisha kwamba tukiyaishi yale tunayoyahubiri kila siku katika majukwaa basi ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania itapiga hatua kubwa sana ndani ya miaka mitano. Ikiwa uongozi wa awamu hii utafanya taratibu nzuri za kusimamia mapato na kuyagawa kwa ustadi mkubwa basi nchi hii itafanya kitu kimoja kinachonukia vizuri kwa mataifa mengine nayo kufanya "reformations" katika serikali zao. Rai yangu inakwenda kwa vijana wa kitanzania ambao wanatumia lugha za "Magufuli ni mbwembwe tu hafiki mbali" mara ooh "rais aliyepita kamweka kwenye mtego wa Zanzibar" au "watendaji wa halmashauri wanapofanya "monitoring" katika maeneo mbalimbali ambapo kuna taasisi za serikali eti ni mbwembwe wataacha tu. "Kauli hizi siyo jengi hata kidogo, muda wa siasa ulishapita hivyo ni kuhahakikisha unakosoa na kutoa mwongozi juu ya nini kifanyike na siyo kupinga alafu hutoi mwelekeo juu ya ninj kifanyike, ukifanya hivyo utakuwa bado unamaumivu ya uchaguzi. Mtanzania wa kawaida unaponunua bidhaa hakikisha unaomba risiti ya malipo ili kodi yako ifike serikalini tofauti na hapo hakuna kitakacho tendeka. Imeandikwa na Mimi John SM Mgejwa ( BA, uchumi na hisabati)

No comments:

Post a Comment