Wednesday, 7 December 2016
EPUKA KUZAA KATIKA UMRI MKUBWA
Hii ni moja ya mambo 34 ambayo matajiri duniani huyakwepa. jambo la kuzaa katika umri mkubwa ni suala lingine ambalo matajiri wengi duniani hujiepusha nalo. Kuzaa katika umri mkubwa siyo chaguo la matajiri walio wengi kabisa. Katika maudhui ya kitabu cha mtanzania mmoja 'Venerando J. Milinga, anashauri kuwa kama umetimiza miaka 42 ni vyema kuacha kuzaa kabisa watoto. Hata kama umebarikiwa mtoto mmoja huna haja ya kuongeza mwingine, kama wewe ni mwanamke, mwandishi wa kitabu anakushauri kuacha kuzaa unapofikisha kati ya miaka 35-40 ili kuweza kupata muda wa kutosha kutekeleza mipango ya maendeleo.
kwa upande wa wanaume, kama umri wako ni zaidi ya miaka 42 na unatamani kupata mtoto hadi sasa, ushauri wake kwako ni kwamba jitahidi ukamwone daktari wa maswala ya uzazi akushauri na uone namna ya kuacha kuzaa watoto. unashauriwa kuzaa watoto ndani ya miaka 20-40 na ukifikisha umri wa miaka 42 huna sababu tena ya kuzaa watoto. tulia ili ufanye kazi za ujasiliamali hasa kusimamia miradi yako badala ya kushughulikia malezi ya watoto wako wadogo.
Jamaa anatoa ushauri huu kwa misingi kuwa endapo utazaa mtoto ukiwa na miaka 42 unakuwa umebakiwa na muda mchache sana wa kuwalea watoto katika kielimu, kiuchumi na kijamii. Mtoto utakaye mzaa ukiwa na umri wa miaka 42 yeye ataanza maisha ya kujitegemea akiwa na miaka 18 ambapo wewe kama mzazi utakuwa tayari una miaka 60 ambao kwa kiasi kikubwa tayari ni umri wa uzee kwa maisha ya sasa. Jamaa anazidi kutoa mfano kuwa ukizaa mtoto una miaka 45, basi utatimiza miaka 60 wakati mwanao ana miaka 15 tu. Umri huo bado ni mdogo sana kiasi kwamba mtoto atakuwa na uhitaji mkubwa wa malezi kutoka kwako wakati na wewe ndo hivyo umri ushakutupa mkono. kitabu kizuri sana. KITABU KINAITWA -MBINU ZA KUPATA PESA NYINGI HADI KUWA BILIONEA. Kitafute kinauzwa 10,000 utajifunza mengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nimefurahishwa sana na uchambuzi wako. Uko vizuri sana katika kuelimisha jamii. Umenukuu kitabu changu kwa usahihi kabisa. Hongera kwa kuendelea kuwajulisha watanzania yale yapasayo kutendwa sasa. Mr. Venerando J. Milinga.
ReplyDelete