Mshambuliaji wa
Barcelona Luis Suarez amekubali kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa
soka nchini Uhispania unaofikia thamani ya Euro milioni 167 ikijumuisha
kipengele cha kumuuza kwa timu itakayomuhitaji.
Taarifa kutoka Barcelona zinasema kuwa mkataba huo utakaomfunga Suarez mwenye miaka 29 mpaka mwaka 2021 utasainiwa siku ya Ijumaa.
Alifunga magoli 40 kwenye ligi kuu soka nchini Uhispania msimu uliopita.
Mshambuliaji mwingine Lionel Messi raia wa Argentina mwenye miaka 29 ana mkataba na klabu ya Barcelona mpaka mwezi June 2018 lakini mazungumzo ya mkata mpya tiyari yameanza.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment