Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameiambia Marekani ijiandae kuondoa wanajeshi wake nchini Ufilipino.
Bwana Duterte amesema huenda akafanyia marekebisho muafaka wa
kijeshi uliyofikiwa kati ya mataifa hayo,ambayo inawaruhusu maelfu ya
wanajeshi wa Marekani kuwa nchini humo kisheria.
Rais huyo hata hivyo ,amesema uhusianao kati ya mataifa hayo mawili huenda ukaimarika chini ya utawala wa Donald Trump
Habari zaidi zinasema matamshi Duterte huenda yamechangiwa na
uamuzi wa Marekani kusitisha msaada wake kwa Ufilipino kufuatia sera
yake ya kuwapiga risasi na kuwaua wahalifu wa ulanguzi wa dawa za
kulevya.

No comments:
Post a Comment