Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli, ameelezea
kusitikishwa kwake na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo jipya kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Gharama hiyo ni ya shilingi bilioni 590, ambayo ni kubwa
ikilinganisha na jengo lililojengwa. Rais Magufuli amesema hayo alipofanya
ziara ya kushtukiza kwenye uwanja huo.
"Hivi kulikuwa na sababu gani za nyinyi wataalamu wa
serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na
bilioni 560," aliuliza Dkt. Magufuli.
Awali mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya
BAM International , alitangaza kusitisha ujenzi huo kutokana na kutolipwa.
Mheshimiwa Rais Magufuli aliahidi kulipa fedha hizo.
Kufuatia hali hiyo Mheshimiwa Rais mafufuli amemuagiza
waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mheshimiwa Prof Makame Mnyaa
aliyeongoza nae kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji
wa mradi huo, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na mkandarasi anayejenga uwanja huo
na Mhandisi mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment