Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Tuesday, 28 November 2017

Siri 39 Ambazo Wengi Zimewasaidia Kuwa Mamilionea



1.  Tafuta fursa kila kona

2.  Tumia kipaji chako


3.  Kuwa na nidhamu katika fedha- matumizi mazur ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka,usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako, nk.

4. Kuwa na nidhamu katika afya yako:Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote-kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara, nk.

5. Usipoteze muda-jali muda kuliko kitu chochote kwa muda ndio kila kitu, muda ni mali.

6. Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali. Huko utakutana na watu mnaoendana kimtazamo, usijaribu kabisa kupiga zogo na watu ambao mara nyingi huwa wanapinga kila kitu wakati wao wenyewe mfukoni hawana kitu.

7. Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato. Kama wewe ni mfanyakazi unategemea mshahara ni lazima akili yako uichuje,  maana maisha ya namna hiyo hayawezi kukufanya uwe milionea.  Hangaisha kichwa chako kuhakikisha kuwa unaongeza vyanzo vya mapato yako kila siku.

8. Tafuta maarifa kwa mamilionea
mbalimbali duniani-soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa. Kama unataka kuwa milionea wachumi hawatarajii kuona wewe mishe mishe  zako zimeegemea kujadili kuongeza nguvu za kiume,  kufuatilia vituko mbalimbali ambavyo havina tija yoyote

9. Jenga urafiki na taasisi za kifedha-mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha-tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri  mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

10. Kuwa na shauku- kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa, usiwe mnyonge kila wakati kwa kuwaza unapoona wenzako wanatengeza pesa,  dumisha shauku yako ya kutaka kuwa milionea.

11. Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. Imani hujenga kujiamini,  mtu anapojiamini katika mambo ya msingi ndivyo hivyo hufikia mafanikio yake bila wasiwasi.

12. Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. Ni aibu kuishi duniani na maisha haya bila kuwekeza kwenye biashara au kwenye miradi mbalimbali.

13. Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa- angalia fursa hapo ulipo na wekeza.

14. Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. Hapa wengi wanashindwa kwa sababu ya mazoea, huwezi kupata fedha alafu usiifanyie bajeti.  Hilo ni kosa kubwa kwa milionea yeyote au mtu yeyote anayetaka kuwa milionea.

15. Chunguza jamii yako wanakosa bidhaa gani kisha dili na bidhaa hiyo nawe utakuwa milionea. Lakini pia uwe na lugha nzuri kwa jamii unayotaka kuiuzia bidhaa.

16. Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha. Hakikisha hilo wazo unaliandika kwenye karatasi kwa sababu kuna mengi tu ya biashara huzaliwa na kufa papo hapo hivyo usipoliandika hakuna unachokifanya.

17. Fanya vitu wewe mwenyewe- acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu. Chukulia mtu ayafanyayo kama mfano kwako lakini usilazimishe kufanya anachofanya yeye maana hujui alianzaje,  fanya kulingana na uelewa wako. Hata kama ukichukua wazo lake lakini lifanye kwa staili yako mwenyewe.

18. Kuwa na malengo- kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo. Malengo ndiyo humchochea mtu katika kufikiri na kugundua kuwa afanye nini ili afikie malengo aliyojiwekea.

19.  Kuwa na moyo wa ujasiri-usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.

20. Karibu na matajiri-usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

21. Mtangulize Mungu-mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

22. Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi, nk.

23. Acha woga-jaribu biashara yoyote woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

24. Kuwa na mtazamo chanya- usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.

25. Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

26. Kuwa na mipaka katika mambo yako-usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni bidhaa zao hawapangiwi na mtu.

27. Dili na watu wenye kipato kidogo na kati katika biashara zako; mamilionea wengi hulenga mahitaji ya watu wa hali ya chini ambao ndio wengi hapa duniani. Baadhi ya mahitaji ya watu wa hali ya chini ni (a)Vyakula na vinywaji (b)Vifaa vya ujenzi (c) Vifaa vya umeme

28. Kuwa mwaminifu-mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

29. Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako-waulize  watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.

30. Kuwa na plani katika kazi zako kila siku. Usiwe mtu ambaye mambo yako hayaeleweki kila kukicha,  ukifanya hivi kwa dhati ya moyo wako lazima ufanikiwe tu.

31. Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe. Kama hutafakari kuhusu ni aina gani ya maisha unataka uishi basi umilionea utausikia tu kwenye habari kuwa fulani ana pesa nyingi. Jitahidi kulenga mbali kwa kuwa na maono ya maisha unayotaka kuyaishi.

32. Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja. Bidhaa siyo lazima iwe ya kubebeka, inaweza kuwa hata kazi ya mtandao hivyo unaweza kuongeza wateja kwa kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

33. Ubunifu ni muhimu sana-fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini-kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu, nk.

35. Nunua hisa katika mabenki, makampuni mbalimbali:Mamilionea wengi hununua hisa hivyo humiliki mabenki na makampuni mbalimbali.

36. Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni.Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli

37. Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea.

38. Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea- kila binadamu anaweza kuwa milionea.

39. Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa- kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu, nk.

HITIMISHO;
Kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani!

No comments:

Post a Comment