Friday, 24 November 2017
Waafrika Tumelogwa, Kumbe Libya Kuna Soko la Watumwa?
FAHAMU Hivi karibuni nchini Libya kumekuwa na tukio la kuwakamata
wahamiaji haramu, na kuwauza kwenye soko la watumwa kwa kupigwa mnada, anayefika bei basi humchukua mtumwa wake na kuondoka naye.
Watu hao ambao wengi wao ni vijana wamekuwa wakitoka nchi mbali mbali za Afrika Magharibi, kutafuta uwezekano wa kwenda nchi za Ulaya kujitafutia maisha.
Baadhi ya vijana ambao wamenusuriwa na biashara hiyo wameelezea kwamba kitendo hiko kinawaumiza sana kuona waafrika wenzao wanakuwa na roho za kinyama na kuwauza kama bidhaa isiyo na thamani.
Mara nyingi watu hao huuzwa kwa dola 400 za Kimarekani ambazo ni sawa na takriban laki 9 za kitanzania.
Umoja wa nchi za Afrika mpaka sasa haujatoa kauli rasmi juu ya vitendo hivyo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu zaidi ya kutaka uchunguzi kufanyika, kitendo ambacho kinalalamikiwa kuwa hawajali.
Nchi ya Rwanda imesema iko tayari kuchukua wahamiaji 30,000 waliopo nchini Libya wakitafuta safari za kwenda Ulaya kwa sababu haiwezi kuvumilia kuona vijana wa kiafrika wakiuzwa kama ng'ombe sokoni.
- Kuna zaidi ya wakimbizi 400,000 nchini Libya wengi kutoka Senegal, Ivory Coast, Chad, Somalia, Eritrea na Ethiopia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment