Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Thursday, 15 December 2016

Binti Atakayeongoza Wamarekani Kuimb Wimbo wa Taifa la Marekani Wakati wa Kuapishwa kwa Donald Trump

Jackie Evancho ni binti wa miaka kumi na sita aliyeshiriki katika mashindano ya American Got Talent ya mwaka 2010, binti huyu alipata umaarufu baada ya kushika nafasi ya pili katika shindano hilo. Alishika namba mbili akiwa na umri wa miaka 10. Binti huyu ndiye atakayewaongoza wamarekani katika kuimba wimbo wa taifa la Marekani siku ambayo rais mteule bwana Donald Trump. Baadhi ya wanamsiki wameanza kutajwa
tajwa ingawa habari hazijathibishwa maana wasanii wengi nchini Marekani wamekuwa wakisusia kushiriki katika kumuunga mkono bwana Trump kwa sababu ya vuguvugu la uchaguzi na maandamano yaliyokuwa yakiendelea nchini Marekani mara baada ya Trump kutangazwa mshindi.
Kanye West na Andrea Bocelli wamekuwa wakidhaniwa kushiriki katika kutumbuiza siku ya kuapishwa rais wa Marekani bwana Donald Trump. Baadhi ya wamarekani wamekuwa wakisema hasa wale wanaomuunga mkono rais wan chi hiyo kuwa mwanadada huyo atawaunganisha wamarekani wote na kurudisha mshikamano wa siku zote licha ya makundi kutokea mara baada ya uchaguzi hasa upande wa Bi Hillary. Tunawatakiwa mema wamarekani wote hasa wanapokuwa wakisubiri kuapishwa kwa rais wao mteule.


 Mtazame chini hapa huyo binti akiimba.


No comments:

Post a Comment