Mtoto wa rais wa zamani wa msumbiji aitwaye Valentina Guebuza aliyetajwa katika jalida la Fobes mwaka 2013 kama mwanamke wa saba kwa kuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika ameuawa kwa kupigwa risasi kadhaa katika mwili wake
. Dada huyu alikuwa ni mtoto wa rais wa zamani wa Msumbiji bwana Armando Guebuza ambaye alistaafu mwaka 2013 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Dada Valentina alifunga ndoa yake na bwana Zorfino Muiuane mwaka 2014, ndoa ambayo ilihudhuriwa na watu takribani 1,700 akiwamo rais wa Afrika Kusini Jackob Zuma. Mme wake tayari yuko kwenye mikono ya dola baada ya tukio hilo kutokea. inasemekana mume wake ndiye amemuua. Mme wake alikamatwa katika eneo la starehe mjini Maputo.
No comments:
Post a Comment