Wananchi
katika mji wa Augsburg nchini Ujerumani jana walijikuta katika mshituko na
mshangao mkubwa, bomu kubwa la vita ya pili ya dunia liligunduliwa katikati ya
mji wa Augsburg, zaidi ya nyumba 32, 000 zenye idadi ya watu wapatao 54, 000
walilazimika kuyahama makazi yao ili kujiepusha na madhara makubwa.
Watu 54,
000 waliondoka katika eneo hilo jana katika asubuhi ya krismasi (Jumapili)
kutoka mji wa Augsburg, Ujerumani. Barabara zote zinazopita katika mji huo
zimefungwa zote toka jumapili tarehe 25 disemba 2016 kuruhusu wataalamu wa
mabomu kulitegua. Bomu hilo lilikuwa limewekwa na taifa la uingereza enzi hizo
za vita, lina uzito wa tani 1.8. Polisi walishindwa kukadiria ni kwa muda gani
wananchi watatakiwa kuwa nje ya makazi yao. Shule za umma zimefunguliwa
kutumika kama makazi kwa wahanga wa eneo hilo.
Mara
kwa mara mabomu ya Marekani na Uingereza yamekuwa yakipatikana katika miji
mbalimbali ya Ujerumanib lakini kwa mara ya kwanza Ujerumani imeshuhudia idadi
kubwa ya watu wakiyakimbia makazi yao tangu vita yenyewe.
Mwaka
2011 bomu jengine lilipatikana katika mji wa Koblenz ambalo lilisababisha watu
45, 000 kuhama kwenye makazi yao. Mataifa mengine ya Ulaya pia mabomu ya vita
ya pili ya dunia yamekuwa yakipatikana sana. Mwaka 2015 bomu la kijerumani liligundulika
nchini uingereza hali iliyopelekea watu 1,500 kuhama makazi yao. Wakati wa vita
ya pili ya duniamji wa Augsburg ulikumbwa na mashambulizi mengi ya mabomu
kutoka kwa waingereza na wamarekani
No comments:
Post a Comment