Saturday, 10 December 2016
Dangote akutana na Rais Magufuli Ikulu leo
Siku kadhaa zilizopita nchini Tanzania kulikuwa na mijadala mbalimbali ambapo hoja iliyokuwa gumzo ilikuwa kuhusu tajiri namba moja barani Afrika ambayo amejenga kiwanda cha saruji nchini Tanzania katika mkoa wa kusini mwa Tanzania uitwao Mtwara. Mitandao ya kijamii, magazeti na vyombo mbalimbali vya habari kama tv na radio vilisikika vikiandika au kutangaza kuwa Dangote anataka kufunga kiwanda chake kwa sababu serikali imekuwa haimjali katika suala zima la mali ghafi za kuendeshea shughuli ya uzalishaji. Pamoja na maneno ya vyombo vya habari, pia viongozi mbalimbali wenye dhamana ndani ya serikali akiwamo waziri wa viwanda Charles Mwijage walitoa kauli mbalimbali kuhusu Dangote mmliliki wa kiwanda kuwa alitaka mali ghafi za bure na maelezo mengi tu, lakini rais wa nchi John Magufuli aliamua kutafuta siku maalumu ili kuongea na huyo tajiri katika ikulu ya nchi, Magogoni Dar es Salaam ambapo leo amekutana na tajiri Dangote kujadili kuhusu biashara yake na kupata ukweli kuhusu ni nini kimetokea hadi kufikia hayo yanayosemwa katika vyombo vya habari. Kulingana na namna ambavyo Dangote kaelezea imeonekana kabisa kwamba vyombo vyetu vya habari haviko makini katika kuandaa taarifa, kwa sababu jamii nzima iliaminishwa hivyo kuwa dangote ananunua malighafi kutoka afrika kusini baada ya kushindana bei na serikali kuhusu makaa yam awe na gesi hali ambayo Dangote kaikanusha na kuongeza kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina mazingira mazuri ya uwekezaji na pia malighafi zake siyo ghali kama vyombo vya habari vilivyoripoti. Dangote aliendelea kusema kuwa tayari ameagiza magari makubwa ya kusambazia cement takribani 600 na wakati naingia mtandaoni tayari meli kuwa kwa mara ya kwanza kabisa imetia nanga katika bandari ya mtwara, meli hiyo inaitwa Morning composer iliyobeba malori ya Dangote yenye kubeba magari 6, 000 imetokea nchi za China na Japan
MAGARI YA DANGOTE YAKIWASILI BANDARI YA MTWARA NA MELI YA MORNING COMPOSER
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment