LIGI kuu Tanzania
Bara inatarajiwa kuendelea tena kesho Ijumaa kwa mchezo Na. 129
utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam utakaochezeshwa na Mwamuzi, Ludovic Charles
kutoka mkoani Tabora akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na.
1) na Alnord Bugado wa Singida (Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa Akiba –
Mezani anatarajiwa kuwa Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.
Jumamosi Desemba 24, 2016
kutakuwa na mechi sita ya Mbeya City na Toto African kwenye Uwanja wa Sokoine
jijiji Mbeya katika mchezo Na. 130 utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa
Dodoma wakati Mwamzi wa kati atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku
wasaidizi wake wakiwa ni Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa
Morogoro. Mwamuzi wa akiba atakuwa Cherles Mwamlima.
Mchezo Na. 131
utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika Uwanja wa Kaitaba,
uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna Nassoroi Hamduni wa Kigoma huku
Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara akisaidiwa na Joseph Masija na Robert
Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani atakuwa Jonesia Rukyaa wa Kagera.
Ndanda itaendelea kubaki
nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na baada ya kucheza na
Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo, safari hii inaikaribisha Mtibwa
Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132 utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe
wa Morogoro wakati Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta
wa Tanga na Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo. Mchezo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru,
kati ya Simba
na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam utasimamiwa na Tito
Haule wa Morogoro na kuchezeshwa na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga akisaidiwa na
Omari Kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid
wa Dar es Salaam atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.
Majimaji ya Songea
itakuwa mwenyeji wa Azam FC ya Dar es Salaam katika mchezo huo ambao
Mwamuzi atakuwa Ngole Mwangole wa Mbeya akisaidiwa na Mirambo Tshikungu na
Mashaka Mwandembwa – pia wote wa Mbeya huku kamishna akiwa ni David Lugenge wa
Iringa. Mwadui atakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya
Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga kwenye mchezo huo Na.
135, utakaosimamiwa na Kamishna Staricko Nyikwa wa Singida na mwamuzi atakuwa
ni Emmanuel Mwandembwa akisaidiwa na Abdallah Uhako na Agnes Pantaleo wote wa
Arusha na mezani anatarajiwa kuwa Ezekiel Mboi wa Shinyanga. Desemba 26,
Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja
wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo Na 136 na
Manyama Bwire wa Dar es
Salaam atakuwa Kamishna wa mchezo huo wakati Mwamuzi ni Forentina Zabron wa
Dodoma akisaidiwa na Hassan Zani wa Arusha na Silvester Mwanga wa Kilimanjaro.
Mwamuzi wa akiba - Mezani atakuwa Andrew Shamba wa Pwani. Desemba 28, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili
ambako Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na. 137 ambako Juma Chiponda wa
Tanga atakuwa kamishna wa mchezo huo. Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakuwa Eric
Onoca wa Arusha akisaidiwa na Michael Mkongwa wa Njombe na Janeth Balama wa
Iringa. Mwamuzi wa akiba atakayekaa mezani atakuwa Mwanahamisi Matiku wa Dar es
Salaam.
Kadhalika siku hiyo,
Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa
Manungu ulioko Mvomero katika mchezo Na. 138 utakaosimamiwa na Kamishna Pius
Mashera wa Dodoma, utachezeshwa na Mathew Akrama kutoka Mwanza akisaidiwa na
Abdallah Rashid wa Pwani na Gasper Ketto wa Arusha. Mwamuzi wa akiba atakuwa
Selemani Kinugani.
Kadhalika
Desemba 29, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Ruvu Shooting ya Pwani
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru Dar
es Salaam katika mchezo ambao mwamuzi atakuwa Alex Mahagi wa Mwanza. Katika mchezo huo
Na. 139, Mahagi atasaidiwa na Ferdinand Chacha pia wa Mwanza na Rashid Zongo wa
Iringa huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Kamishna
wa mchezo atakuwa Peter Temu wa Arusha.
Azam itavaana na Tanzania
Prisons ya Mbeya katika mchezo Na. 140 utakaosimamiwa na Elizabeth Kalinga wa
Mbeya huku Mwamuzi akiwa ni Jimmy Fanuel wa Shinyanga huku wasaidizi wake
wakiwa ni Makame Mdog pia wa Shinyanga na Abdallah Mkomwa wa Pwani huku Kassim
Mpinga akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna anatarajiwa kuwa Nassib Mabrouk wa Mwanza na Mwamuzi ni Isihaka
Mwalile na wasaidizi wake ni Hellen Mduma na Omary Kambangwa – wote kutoka Dar
es Salaam. Julius Kasitu wa Shinyanga anatarajiwa kuwa Mwamuzi wa Akiba.
Kadhalika
siku ya funga mwaka, Mbeya City inatarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya katika Mchezo Na. 143 ambao msimamizi wa mchezo atakuwa
Joseph Mapunda wa Ruvuma. Mwamuzi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Hussein
Athuman wa Katavi wakati wasaidizi wake watakuwa ni Lulu Mushi wa Dar es Salaam
na Nicholaus Makaranga wa Morogoro. Mwamuzi wa Akiba Mezani atakuwa Mashaka
Mwandembwa wa Mbeya.
Januari mosi kutakuwa na
michezo miwili tu ya kukaribisha Mwaka Mpya ambako Toto African ya Mwanza
itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika
mchezo Na. 144 utakaosimamiwa na Jovin Bagenda wa Kagera. Mwamuzi atakuwa
Israel Nkongo sambamba na wasaidizi wake Soud Lila na Frank Komba, wote wa Dar
es Salaam. Mwamuzi wa akiba mezani atakuwa Mathew Akrama wa Mwanza.
Pia African Lyon ya Dar
es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu katika mchezo Na. 142 utakaofanyika
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kamishna atakuwa Hamisi Kitila wa Singida
wakati Mwamuzi anatarajiwa kuwa Selemani Kinugani wa Morogoro wakati wasaidizi
wake ni Omary Juma wa Dodoma na Agnes Pantaleo wa Arusha wakati mezani atakuwa
Shafii Mohammed wa Dar es Salaam. Mara baada ya michezo hiyo, Ligi Kuu ya Vodacom itasimama kwa wiki
mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari mosi,
mwaka 2017
Chanzo: Michuzi BLOG
No comments:
Post a Comment