Saturday, 10 December 2016
Majasusi wa CIA nchini Marekani wamesema Urusi ilidukua uchaguzi, Obama naye afunguka
Nchini Marekani majasusi wa CIA wamesema kuwa wana uhakika mkubwa kuwa taifa la Urusi lilifanya udukuzi kkatika emails za bibi Hillary Clinton aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha republican. Pia kwa taarifa zilizochapwa na gazezi la New York times na Washington Post zinaeleza kuwa Urusi walishiriki katika udukuzi kwa mgombea wa democratic ili kumsaidia Donald Trump aliyefanikiwa kushinda uchaguzi. Kufuatia hali hiyo, rais wa Marekani Barack Hussein Obama ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika ili kuhakikisha kama ni kweli Urusi walihusika. Wakati wa kampeni maafisa wa Urusi walisema kuwa hawajamuunga mkono mtu yeyote wakati wa kampeni na bado wameendelea kusema kuwa hawakudukua emails za Mama Hillary Clinton na mshauri wake.
Kwa upande wa pili, maafisa wa kampeni ya bwana Trump (republican) wameendelea kupuuza tuhuma hizo. Trump mwenyewe amesema wanaosema kuwa Urusi ilidukua uchaguzi ni wale wale walioisingizia nchi ya Iraq kuwa ina silaha zilizopigwa marufuku hadi ikapelekea kuuawa kwa rais wa nchi hiyo. Kulingana na kauli ya rais wa Marekani naweza kusema tutarajie mambo mengine mapya ambayo hatujawahi kuyaona na kuyasikia katika historia ya Marekani toka ipate uhuru mwaka 1776 kutoka kwa mwingereza.
Wiki kadhaa zilizopita, wananchi kadhaa wa Marekani waliandamana huku wakipinga kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa rais wa Marekani, wengi wao walipinga kuchaguliwa kulingana na matamshi yake ya kuogofya aliyokuwa akiyatoa wakati wa kampeni kwa makundi mbalimbali ya watu nchini humo, mfano; wahamaiaji haramu, ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico, waislamu nk. Dunia nzima inaombwa kuliombea taifa la Marekani ili lisijekugawanyika na baadhi ya majimbo kama California yakajitenga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment