Friday, 9 December 2016
Wasomi badilikeni kifikra ili Taifa lisonge mbele
Na John Mgejwa,
Kwa nini unapopata digrii unajiona mtu wa juu sana na unaeamini kwamba unaweza kila kitu? Mbaya zaidi unaamini kuwa ambao hawajasoma hawajui chochote na kuwa wanafanya mambo yao bila kufikiri. unadiliki kujiona wa tofauti sana ukiamini kwamba digrii yako itakupa kila kitu, hadi zile kazi za kukuingizia kipato unazikataa eti kisa zinahitaji nguvu zaidi- physical na siyo soft. mtu wa ngazi ya astashahada na stashahada hakwaambii kitu na ukakubaliana nacho hata kama kina manufaa!! Dunia hii ina kazi hasa ya kubadilisha minds za wasomi.
Digrii sasa ni utajiri katika fikra za baadhi ya wasomi, ukienda vijiweni utawakuta watu wa digrii, na ukitaka kumjua wewe kaa kimya kwa muda bila kuzungumza chochote utamjua tu, utamjua siyo kwa kuonyesha utaalam fulani ila kwa kujigamba kuonyesha ana digrii, aliyefeli mitihani anatazamwa kama mtu asiye na lolote kwa baadhi ya wenye digrii yaana ni full kushushiana hadhi. baadhi ya wenye digrii wanaamini kila kazi ya kiofisi anaiweza yeye tu. na ndiyo maana utasikia mtaani " wamechukua wa diploma wakaniacha mimi niliye na digrii" kauli hizi zinanitia wasiwasi kwa mtu mmoja mmoja kujiletea maendeleo! inamaana mtu wa diploma hawezi?
Jiulize kwa nini wasomi wa digrii maisha yao siyo mazuri sana ukilinganisha na wafanyabiashara ( wajasiliamali) hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya walio na digrii wanachukulia digrii kama title ya kumpaisha mtaani, kwa majirani nk. Kwa ufupi, wasomi wamekuwa wabinafsi sana nah ii ni kutokana pia na dhana ya “ficha kazi yako mwenzko asiangalizie”, wasomi wanapomaliza vyuo huitumia hiyo mbinu hata kwa watu wao wa karibu, msomi hayupo tayari kumdokezea mwenzake mbinu zianzotambulika kisheria za kujipatia maendeleo.
Usimdharau mtu kisa una digrii na yeye hana, Billgates ambaye ni tajiri wa kwanza Amerika na duniani anasema alifeli baadhi ya mitihani yake, rafiki yake alifaulu mitihani yote na sasa ni mhandisi ktk Kampuni ya Microsoft, cha kushangaza hiyo microsoft inamilikiwa na billgates! kuna inverse relationship kati ya maendeleo na kufeli mitihani ya darasani, sasa wewe kama unamdharau unayemzidi elimu ni bora urudi darasani tena maana bado hujaamka kifikra.
Kupata digrii haimaanishi umefukuza umasikini bali ni zana unayoweza kuitumia kufukuza umasikini na tusipokuwa makini tutakuwa masikini zaidi ya tulivyokuwa mwanzo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment