Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Saturday, 17 December 2016

Mkongwe wa Soka Ibrahimovic Alivyo Wachosha Wachezaji wa West Bromwich Kwenye Uwanja wao




Zlatan Ibrahimovic (35) ameendelea kuing'arisha timu ya Manchester United baada ya kusuasua sana kwenye ligi kuu ya uingereza.

  Ibrahimovic ameifungia timu yake ya sasa (Man U) magoli mawili yaliyopatikana katika dakika ya 6 na 56 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa nunge. Mahojiano yaliyofanyika na kocha wa manchester united Jose Morinho amesema kuwa timu yake imecheza vizuri na anahukuru tu kwamba wanaendelea kuongeza pointi katika msimamo wa ligi. Morinho alipoulizwa kuhusu Zlatan alisema anafurahi kwamba anafunga na wameongeza pointi na kufika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi

No comments:

Post a Comment