Rais
mteule wa Marekani ameiambia Israel kukaa imara hadi pale atakapochukua mamlaka
mwezi ujao.
Pia
amesema kuwa Israel imekosewa heshima na kwamba hilo lazima lisitishwe.
Ni
matamshi yake ya hivi karibuni katika mtandao wa kijamii wa Twitter.
Wakosoaji
wamemwambia rais huyo mteule kutumia njia rasmi za kuwasiliana kuhusu maswala
ya kimataifa.
Siku
ya Ijumaa, Marekani iliamua kutoshiriki katika kura ya veto kuhusu uamuzi wa
Umoja wa Mataifa unaokataza Israel kuendeleza ujenzi wa makaazi katika maeneo
ya Palestina inayokalia.
Katika
machapisho ya mtandao wa Twitter siku ya Jumatano mjini New York, Bw Trump
alisema: Hatuwezi kuruhusu Israel kutoheshimiwa. Marekani ilikuwa rafiki mkubwa
wa Israel ,lakini sio tena. Mwanzo wa kumalizika kwa urafiki huo ni pale
Marekani ilipokubali kuingia katika makubaliano na Iran, na sasa Umoja wa
Mataifa ! Kaa imara Israel,tarehe 20 mwezi Januari inakaribia!
Zaidi
ya Wayahudi 500,000 wanaishi katika makao 140 yaliojengwa na Israel tangu
uvamizi wake 1967 ambapo walikalia maeneo ya West Bank na mashariki mwa
Jerusalem.
Makaazi
hayo sio halali kulingana na sheria ya kimataifa ,ijapokuwa Israel inapinga
hilo.
No comments:
Post a Comment