Na John S.M Mgejwa
Chanzo cha umasikini Tanzania ni kitu special kilicho ndani ya akili za watanzania ambacho kinazidi ufisadi na rushwa na uozo wa vyama vya siasa.
Chanzo cha umasikini Tanzania ni kitu special kilicho ndani ya akili za watanzania ambacho kinazidi ufisadi na rushwa na uozo wa vyama vya siasa.
Tunafahamu fika kwamba viongozi wana kazi ya ziada ambayo
walitwishwa na wananchi wao kusimamia rasilimali zote za taifa, lakini hali
imekuwa tofauti kwa Tanzania ingawa dunia inaamini hivyo kuwa usimamiaji mzuri
wa rasilimali na utoaji fursa kwa wananchi ndiyo njia madhubuti ya kuleta
maendeleo.
Ifike mahali watanzania tushtuke kwamba kuna kitu ambacho
kiko juu ya hayo yanayoaminiwa duniani kuwa ndiyo chanzo cha maendeleo. Kwa
muktadha huo ukiwa kama mtu unayehangaisha akili yako kufikiri kila kukicha
katika hali ya sasa hutakiwi kabisa kulaumu kiongozi kwamba ndo anasababisha
wewe uwe masikini. Nina sababu zifuatazo zinazoonyesha kuwa watanzania
tunaendelea kuwa masikini kwa sababu ya kitu ambacho kipo ndani ya akili zetu
ambacho kimewashinda viongozi kukisimamia maana mtanzania wa kawaida ukiwa
"complex" katika kusimamiwa na kukupa siri za ushindi basi kwako
kiongozi hatakuwa na maana hivyo hali itabaki kama ilivyo kila kukicha.
1. Mtanzania ana uwezo wa kumiliki iPad ya sh.1,000,000,
simu ya laki 400, 000/ , 250,000 etc lakini bado anao uwezo wa kulaumu na
kulalamika kuwa hana mtaji sasa hivi angekuwa mbali, hili tatizo linasababishwa
na kile kitu special ambacho kimo ndani ya akili yake ambacho hata awe kiongozi
wa namna gani hawezi kumletea maendeleo hadi pale mtanzania huyu atakapoondoa
hicho kitu special ndani ya akili yake.
2. Mtanzania anauwezo wa kuunga bundle la 1000, 2000, kwa
kwa siku , zidisha kwa siku thelathini alafu uzidishe kwa siku mia tatu sitini
na tano (mwaka mzima) lakini bado anao uwezo wa kulalamikia viongozi wake eti
hana kitu na maisha ni magumu, huu ni ujinga ambao unatakiwa kukomeshwa na yeye
mwenyewe siyo kiongozi tena.
3. Mtanzania anao uwezo wa kukata tiketi ya kutoka mwanza
hadi Dar es salaam kwenda kumsalimia Shangazi, kaka , baba Mdogo nk au wakati
mwingine kwenda kuzurura tu na kulifahamu jiji ilhali hapo alipo hana kazi
yoyote , wala afikirii kuwa hiyo nauli angeifanyia mambo ya kumwingizia kipato.
Itifaki imezingatiwa kwa wale wa mwanza ila mtu anaweza kusafiri kwenda mkoa
wowote
4. Mtanzania anao uwezo wa kuwa hewani kuanzia asubuhi hadi
SAA nane usiku aki comment picha za warembo na za handsome boys kila siku huku
akisubiri dona maskani liive atoboe then aendelee kuchati.
5. Mtanzania anauwezo wa kuhakikisha leo anunue nguo gani na
achubue vipi ngozi ili atokelee vizuri zaidi , hapa anatumia pesa siyo mawe
lakini analia hana mtaji.
6. mtanzania anauwezo wa kiakili kujiuliza namna gani ya
kuongeza nguvu za kiume na kuwapata warembo lakini mtakosana sana ukimwambia
hiyo nguvu aitumie kutafuta pesa. Asilimia kubwa ya watanzania wanawaza na
kujadili namna ya kumfikisha mwanamke kileleni na wanawake nao wanatumia kiasi
kidogo walicho nacho kutengeneza makalio ili ngono ishamili zaidi na ukitaka
kugombana naye mwambie atafute pesa au hiyo pesa bora angeanzisha
"firm" Fulani ili imwingizie kipato kuliko kuongeza ukubwa wa kalio
7. Wasomi wengi wanatoka vyuoni wakiwa wamekomaa katika
ubinafsi na hii ni kutokana na mfumo unaotumika mashuleni wa kufanya mitihani
kwa kila mmoja huku akificha kazi yake ili mwenzake asiibie, kumbe Hali hii
huendelea kwa zaidi ya miaka 16 hali ambayo huwafanya wasomi wengi wa tz na
kwingineko kushindwa kuhimili vishindo vya mtaani kwani mtaani wanastaili
nyingine ya maisha ambayo huhusisha kusaidiana na kushirikiana hata kwa
mipango, mpango wako ni mpango wangu ilimradi tupate maendeleo . kumbe utokapo
chuoni unatakiwa uache tabia za ujibuji mitihani kwani zitakufanya uishi maisha
ya usiri sana kwa kila unachofanya utakuwa peke yako.
8. Mtanzania yuko tayari kubagua kazi kisa yeye ni msomi_
hili siyo tatizo la viongozi ni lako, usomi utakuwa bure kama unafikiri kupata
pesa ni elimu basi ujue bado kuna tatizo katika kufikiri kwako.
Ukiangalia mambo hayo yote yanakugusa wewe mwenyewe siyo
mwanasiasa na mbaya zaidi yako kwenye akili yako ambapo solution yake hadi wewe
mwenyewe ujishtukie kwnza. Lucky Dube alisema hivi;
"I can sit here and teach you every trick in the book but at the end of the day it is your life. Good things come to those who got out and made them happen, they don't come to those who wait."
Tatizo tuko nalo sisi kwenye akili siyo ufisadi maana ufisadi pia unasababishwa na hilo tatizo lililo ndani ya akili ya huyo fisadi.
"I can sit here and teach you every trick in the book but at the end of the day it is your life. Good things come to those who got out and made them happen, they don't come to those who wait."
Tatizo tuko nalo sisi kwenye akili siyo ufisadi maana ufisadi pia unasababishwa na hilo tatizo lililo ndani ya akili ya huyo fisadi.
No comments:
Post a Comment