Bahati Bukuku akizungumza kwenye
cha Kikaangoni alisema wimbo wake wa 'Dunia haina huruma' si kama
alimwimbia huyo aliyekuwa mume wake bali anakiri kuwa ni kisa cha kweli
kilichotokea lakini hayo mambo aliyekuwa mumewe alikuwa hayafanyi.
"Aliyewahi kuwa mume wangu
hakufanya hilo tukio ila kile kisa ni kweli kilitokea sehemu, lakini aliyekuwa
mume wangu hakuwa na matatizo haya, ila tu katika harakati zetu za maisha kuna
kupishana hivyo nilipishana naye tu. Siwezi kuongea uongo kwa mtu aliyekuwa
mume wangu, hata nikiandika kitabu siwezi kuruka hili popote nikisimama
nitasema niliolewa ndoa ikanishinda" alisema Bahati Bukuku
Kuhusu skendo kuwa ndoa nyingi za
"watu wa dini" hazidumu, Bahati amesema wanaume wengi wanakosea
kufikiri kuwa wakioa wanawake ambao ni watu wa dini au watu wa injili kama
yeye, wanakuwa wameoa watu wasio na makosa..
"Wengi hudhani ukioa mtu wa
kanisani umeoa malaika ambaye hakosei, sasa wakishaanza maisha anakuta tofauti,
hapo ndipo ndoa inaweza kuvunjika, jama hata sisi ni binadamu pia" Alisema
Bahati
Baadhi ya mashabiki walitaka kujua
endapo alipata watoto katika ndoa hiyo, ambapo Bahati alikataa kuongea chochote
kuhusu yeye kuwa na watot au la, na kusema kuwa hayuko tayari kuongea chochote
huku akisema kuwa ana watoto wengi
"Hili swala la watoto sitaki
kuzungumzia, mimi nina watoto wengi tu, kwahiyo kwenye ndoa yangu nisingependa
kuongelea swala la watoto" alisema Bahati
Mbali na hilo Bahati Bukuku anasema
watu ambao walimzushia kifo ni watu wake wa karibu ambao anafanya nao kazi na
huenda walifanya hivyo ili kutaka kumpunguzia mashabiki wake.
"Walionizushia kifo ni watu
ambao nafanya nao kazi, walidhani watanipunguzia mashabiki lakini pia ni kazi
ya shetani hiyo, hivyo walijifanya ile taarifa imeanzia Congo lakini ni wa
hapahapa ila mamlaka za mawasiliano bado zinaendelea kufuatilia ingawa mpaka
sasa tayari wameshafahamika" alisema Bahati Bukuku
Katika hatua nyingine, Bahati amesema
hivi sasa anaandaa movie ambayo pia itakuwa na lengo la kuinjilisha, na
kufikisha ujumbe wa Mungu kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye uimbaji.
"Kwanza kabla sijatoa wimbo
mpya, natoa filamu yangu mpya inayoitwa 'Mwalimu wa Ndoa', ambayo baada ya wiki
moja itakuwa madukani, niliipeleka BASATA, tayari wameshaipitia, ina mafundisho
mengi mazuri kuhusu ndoa, nawashauri wanawake, mabinti wote waitafute"
Amesema Bahati huku akisita kutaja mastaa walioshiriki katika movie hiyo.
No comments:
Post a Comment