VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi na Mgombea Ubunge
wa Jimbo la Mtama, Selemani Mathew na Katibu wa Chadema Kijiji cha Nyangamara
‘A’ mjini Lindi, wamehukumiwa kifungo cha miezi minane jela bila ya faini
kutokana kufanya mkutano bila ya kibali cha Jeshi la Polisi katika kijiji hicho
wilayani Lindi.
Viongozi hao waliohukumiwa ni kati ya
viongozi sita waliokamatwa na kutuhumiwa kufanya mkutano bila ya kibali cha
Jeshi la Polisi nchini.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi mkoani Lindi, Muhini alitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza mashtaka
pande zote mbili na kubaini viongozi hao walitenda kosa la kisheria.
Tukio lililotokea Aprili 3, mwaka
jana kwa viongozi na wanachama kwa pamoja kufanya mkutano bila ya kibali cha
Jeshi la Polisi wilayani Lindi.
Alitaja kifungu cha sheria
kilichovunjwa ni Kipengele 74(1) na 75 kinachozungumzia Mwenendo wa Makosa ya
Jinai kinachosomeka kwa pamoja na sheria ya Jeshi la Polisi.
Alisema washitakiwa wengine wanne
wanaachiwa huru, kwani walibainika hawana hatia. Hao ni Bashiru Rashidi,
Hassani Mchilima, Abdallah Mmasikini na Isimael Kupilila.
Akizungumzia hukumu hiyo, Mratibu wa
Wanawake wa Chadema Mkoa wa Lindi, Sina Kikuwi alisema mahakama haikutenda haki
kwa watuhumiwa hao.
Alisema taarifa walikuwa nayo kwenye
vikao hivyo vya ndani havihitaji kibali, bali kutoa taarifa ambazo
zilishatolewa katika mamlaka husika.
Selemani Mathew aliwahi kuwa Diwani
wa Vijibweni wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM.
Aligombea katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi mwaka juzi, ambapo katika kura za
maoni za CCM alishindwa na Nape Nnauye.
Baadaye alihamia Chadema ambako
alikuwa mgombea ubunge wa chama hicho, lakini pia alishindwa na Nape ambaye
sasa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
No comments:
Post a Comment