Maandalizi ya sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Marekani, Donald Trump yanaendelea. Miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo ni mwimbaji maarufu wa muziki wa pop kutoka Uingereza, Rebecca Ferguson.
Hata hivyo katika hali ambayo haikutarajiwa na waandaaji wa sherehe hiyo, mwimbaji Rebecca ametoa sharti lenye utata ili aweze kukubali mwaliko huo.
"Nitakubali mwaliko wenu endapo tu nitaruhusiwa kuimba wimbo wa 'Smart Fruit'." Huu ni wimbo wenye maneno yanayopinga ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi nchini Marekani ambao kwa mara ya kwanza ulianza kupata umaarufu miaka ya mwishoni ya 1930.
Pamoja ba kuwajibu kwa maandishi waandaaji wa sherehe hiyo, aidha Rebecca ameandika katika akaunti yake ya Twitter kuwa "Nimealikwa kuimba katika sherehe ya kumuapisha Trump lakini nami nimewaomba waniruhusu kuimba wimbo wa "strange fruit". Wimbo huu una umuhimu mkubwa katika historia ya mapambano ya mtu mweusi nchini Marekani. Najua Marekani hawautaki na ndio maana waliupiga marufuku lakini ni muhimu kuwakumbusha madhara ya ubaguzi wa rangi, hasa dhidi ya watu weusi."
"Pamoja na tofauti zetu, ni muhimu sana tukapiga vita ubaguzi wa rangi. Na mbaya zaidi ni kwamba Marekani wana nafasi ya kupiga vita hili lakini kwa sababu wanazozijua wao hawafanyi hivyo," amesema Rebecca Furgerson.
No comments:
Post a Comment