TAREHE
12/12/2016
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA
TEKNOLOJIA ILITANGAZA KUWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA
SHAHADA ZA UALIMU KATIKA MASOMO YA SAYANSI (FIZIKIA, KEMIA, BIOLOJIA) NA HISABATI WA MWAKA 2015 WAWASILISHE VYETI VYAO
KWA
AJILI
YA UCHAMBUZI WA WAHITIMU WENYE SIFA.
WAHITIMU
WALIOKUWA NA MAPUNGUFU KATIKA
NYARAKA ZAO WANATAKIWA WAWASILISHE TENA. WAHITIMU HAO NI KAMA IFUATAVYO:-
(1)
WALIOTUMA NAKALA ZA “RESULTS SLIPS” AU “ACADEMIC TRANSCRIPTS” BILA NAKALA ZA
VYETI HALISI VYA KIDATO CHA 4, 6,
STASHAHADA AU SHAHADA
(2)
WALIOTUMA NAKALA ZA VYETI VYA STASHAHADA ZA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION
– PGDE) BILA NAKALA ZA “VYETI VYA SHAHADA YA KWANZA PAMOJA NA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZAKE;
WAHITIMU
AMBAO HAWAKUTUMA KABISA NAKALA ZA VYETI VYAO WANAPEWA FURSA YA MWISHO KUTUMA.
WAHITIMU
AMBAO NYARAKA ZAO ZILIWASILISHWA MAJINA YAO YANAPATIKANA KATIKA LINK HIZI .
Kuona orodha bofya hapa chini
WAHITIMU
WALIOPO KWENYE ORODHA HAPO JUU WASIWASILISHE NYARAKA HIZO TENA.
UTARATIBU
WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-
1.
WAOMBAJI LAZIMA ‘WA-SCAN’ VYETI
HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES - KIDATO CHA
4, 6, STASHAHADA, STASHAHADA YA UZAMILI AU SHAHADA) NA
SIYO KIVULI CHA CHETI
(PHOTOCOPY) ;
2.
WAOMBAJI WA STASHAHADA YA UZAMILI
(PGDE) NA SHAHADA LAZIMA ‘WA-SCAN’
NA KUTUMA NAKALA ZA “ACADEMIC
TRANSCRIPTS” ZA SHAHADA YA KWANZA.
3.
WAOMBAJI LAZIMA WAWEKE NAKALA ZA
VYETI VYAO VYOTE KWENYE ‘FILE’
MOJA LIKIWA KATIKA ‘PDF’ NA LIPEWE
JINA LA MWOMBAJI HUSIKA KABLA YA KUTUMA. NYARAKA ZITUMWE KUPITIA ‘BARUA PEPE’
ZAO WENYEWE NA SIYO ZA WATU
WENGINE.
TANBIHI:
1.
WAOMBAJI WATUME TAARIFA ZAO KUPITIA
BARUA PEPE YA WIZARA info@moe.go.tz
2.
TAREHE YA MWISHO KUPOKEA NYARAKA NI 17
JANUARI,2017.
3.
BARUA PEPE ZA KUWASILISHA NYARAKA ZA
WAOMBAJI ZITUMWE MARA MOJA TU NA
SI KWA KURUDIA RUDIA ILI KUEPUKA
USUMBUFU WA KUTAFUTA ZILIZO SAHIHI.
IMETOLEWA
NA
PROF.
SIMON S. MSANJILA
KAIMU
KATIBU MKUU
12/01/2017
No comments:
Post a Comment