Ufaransa inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais mwezi Aprili mwaka huu ambapo wagombea kadhaa wamejitokeza.
Hata hivyo katika hali ambayo isiyotarajiwa na wengi, wananchi ambao
hawaridhiki na wagombea waliojitokeza wameanza harakati za kufungua
mashtaka ili kuitaka Mahakama Kuu ya nchi hiyo kutoa kibali cha Rais
mstaafu wa Marekani, Barack Obama kugombea nafasi hiyo.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la OBAMA17 inaenda sambamba na kutafuta
saini za waungaji mkono 1,000,000 wa azimio hilo litakaloruhusu mashauri
ya raia asiye raia wa Ufaransa kugombea nafasi ya Rais wa nchi hiyo
kuweza kusikilizwa. Hadi jana zaidi ya watu 500,000 walikuwa wamesaini
kuunga mikono azimio hilo.
Maeneo mbalimbali nchini ufaransa yamepambwa na mabango yanayohamasisha mpango huo yenye kauli mbiu isemayo 'Oui on peut', ikimaanisha 'Yes we can'.
Wafaransa wanaounga mkono azimio hilo wanasema Rais mstaafu Barack Obama ana sifa za kuongoza Taifa lolote duniani.
Aidha, wanaotetea hoja hiyo wanasema huu ni wakati wa kutafuta watu wenye uwezo ambapo kigezo cha uraia hakina mantiki kwani kwa miaka migi viongozi raia ndio wamekuwa wanaididimiza Ufaransa.

No comments:
Post a Comment