Friday, 10 November 2017
DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto amewataka watoa huduma na mafunzo kuhusu lishe bora yaanzie ngazi za shule ya msingi ili kuwajenga watoto kuzingatia mlo bora katika kukuza afya za watanzania.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
“Walimu wawe sehemu ya afua za kufundishia wanafunzi juu ya lishe bora hasa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili kuwajengea mazoea watoto kupenda kula mlo ulio bora hata wanapokuwa majumbani mwao” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha,Dkt. Ulisubisya amesema kuwa baadhi ya watoto walio vijini na mijini wana utapia mlo kwa kukosa chakula kilicho bora hivyo jamii inatakiwa izingatie lishe bora ili kuimarisha afya za watoto nchini.
Mbali na hayo Dkt. Mpoki amesema kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawe kipaumbele katika kutoa elimu ya lishe bora ili kuweza kujikinga na Unyafuzi, Kwashakoo na magonjwa yasiombukiza kama vile Kisukari,shinikizo la damu ,magonjwa ya moyo yanayotokana na ulaji kupitakiasi.
Kwa upande wake Meneja wa Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe ECSA Bi. Rosemary Mwaisaka amesema kuwa wameamua kuandaa vitini na vitita vya kufundishia lishe bora ili kuweza kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili ku/kisha elimu hiyo kwawalengwa.
“Tumeamua kuandaa vitini hivi ili viweze kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kuweza kuwafundisha wanajamii juu ya umuhimu wa kula mlo bora na vitatumika Kenya,Uganda na Tanzania” alisema Bi. Mwaisaka.
Naye Mshiriki wa Mafunzo ya Lishe bora kutoka ECSA ambae pia ni Mtoa huduma Bi. Evelyne Minja amesema kuwa mafunzo hayo
yamewasaidia kutoa huduma katika jamii kuhusu mlo bora hasa kwa watoto vijijini na mijini.
“Mafunzo haya yametufanya tujue jinsi ya kuwahudumia na kutoa ushauri juu ya mlo bora hasa kwa watoto wenye viashiria vya utapia mlo kwa kuwapima na kuwapangia vyakula vinavyostahili” alisema Bi. Minja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment