Friday, 10 November 2017
TAWLAE Kuunganisha Wakulima na Tafiti
Chama cha Wanawake Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Mazingira, Tanzania Association of Women Leaders in Agriculture and Environment ( TAWLAE)
leo wamefungua rasmi mkutano wa mwaka wa 21 ambao mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bi Butano Philipo kwa niaba ya Waziri wa Mazingira Mhe. January Makamba, mkutano ambao umefanyika leo katika Viwanja vya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti ya Chama cha Wanawake Viongozi katika kilimo na mazingira Dkt. Sofia Malote amesema, Lengo kubwa la mkutano huo ni kuunganisha wakulima na tafiti mbalimbali zilizoandaliwa na wataalamu hao.
Maadhimisho hayo ya 21 yamebeba kaulimbiu isemayo Uchumi wa Viwanda Tanzania Wanawake tupo tayari, hapa kazi tu.
Aidha Dkt. Sofia Malote amesema kazi ya TAWLAE ni kuwaunganisha wakulima wadogo au wakubwa na tafiti mbalimbali ambazo zimetafitiwa hapa nchini ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa watanzania katika kilimo.
Akizungumza katika wasilisho lake Dkt. Malote amesema kilimo kilikuwa na faida ndogo kwa sababu utalaamu, teknolojia na juhudi zilikuwa bado hazijatumika vizuri kwenye kilimo hivyo ni jukumu la TAWLAE kuhakikisha kuwa wanaleta mapinduzi ya kilimo katika uchumi wa viwanda.
Ili kuingia katika uchumi wa viwanda ni lazima uzalishaji wa kilimo uwe na tija, kuwepo na uboreshaji wa masoko na teknolojia ambapo wataalamu wanawake ndio wanajukumu kubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo alisema Dkt.Malote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment