Habari motomoto zilizojili hivi punde kutoka kila kona ya Dunia

Thursday, 30 November 2017

HUWEZI AMINI, LAKINI UKWELI NI KWAMBA DUNIANI NI KUKAZA ROHO TU


Hakika maisha ni mapito,  aliyesema msemo huu hakukosea kabisa. Katika maisha mara nyingi huwa ni kupanda na kushuka.

Ndivyo ilivyo kwa msanii wa kizazi kipya,  msanii mkongwe ambaye alishirikiana na Joseph Haule (Prof. Jay)  kuifundisha jamii kuhusu ukweli halisi wa maisha ya mtu aliyeathirika na ugonjwa wa Ukimwi na namna ya kumsaidia aishi bila mawazo kabisa.

Ferouz ni kati ya wasanii waliojaliwa na Mwenyezi Mungu katika vipaji.  Akiwa kinara wa kuimba nyimbo zinazofikirisha kwa huzuni kubwa.

Msanii huyu alipotea kwenye ulimwengu wa muziki kwa kipindi kirefu kidogo, inasemekana alihamia kwenye biashara ya madini ambayo yeye anasema kuwa ulimuingiza hasara kubwa na hatimaye watu kuanza kumjadili kuwa amefulia.

Hakika hili pia limejidhihirisha katika video ya wimbo wake mpya., anadai hata marafiki wake wa muda mrefu wamekuwa hata hawapokei simu yake anapowapigia.

Ferouz anakiri kuwa duniani jifunze kukaza roho,  usipofanya hivyo basi Jiandae kuzikwa mapema kwa magonjwa ya moyo.  Ferouz anasema wasanii wenzake
walimtenga sana baada ya kusikia kuwa aliingia hasara.

Ferouz katika wimbo wake huo mpya anaonekana mtu wa dhiki,  dhiki ambayo siyo ya kuigiza bali ni hali halisi ya maisha yake baada ya kufilisika kwa sababu ya biashara ya madini iliyochukua pesa zake nyingi na akajikuta hana chochote.

Ametoa wimbo mzuri,  wimbo wenye mafundisho mengi kwa ulimwengu wa sasa.  Ni vizuri ukausikiliza na kuutazama huu wimbo wake mpya. Anasema amejifunza mengi na ameamua kurudi katika fani yake hiyo ya uimbaji kwa nguvu mpya.
Bonyeza hapa chini kuusikiliza




No comments:

Post a Comment