Friday, 10 November 2017
SAKATA LA LISSU, SAANANE LALICHEMSHA BUNGE
Dodoma. Sakata la kushambuliwa kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, kuuawa kwa mwenyekiti wa chama hicho mkoani Geita,Alphonce Mawazo na kutoweka kwa Ben Saanane jana liliibua tuhuma tofauti baada ya kuibuliwa tena bungeni.
Sakata hilo liliibuliwa na kiongozi wa kambi ya upinzani, Freeman Mbowe aliyetaka kujua sababu za serikali kuonekana inachelewa kufanya uchunguzi na kujibiwa kuwa vyombo vya dola vinalishughulikia kama linavyochunguza mauaji ya viongozi wa vijiji katika wilaya ya mkoa wa Pwani na vitatoa taarifa.
Lakini mbunge wa ulanga (CCM), Goodluck Mlinga akaomba mwongozo wa spika, akimtuhumu Mbowe kukiuka katiba kutokana na kutaka uchunguzi wan je wa mashambulinzi na mauaji hayo, lakini baadaye akakumbana na ombi la mbunge wa chadema kutaka Mlinga ahusishwe na shambulizi dhidi ya Lissu kwa kuwa alishawahi kuhusishwa kwa mauaji.
‘Sinema’ ilianza kwa Mbowe kumuuliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu matukio hayo dhidi ya viongozi wa Chadema, akisema serikali haijachukua hatua yoyote.
Mbowe alihoji hayo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye aliendelea kusisitiza kuwa serikali inaviamini vyombo vyake vinavyoendelea na uchunguzi na kwamba hakuna haja ya kuita wachunguzi kutoka nje.
“Tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa nia ya kuua kwa mheshimiwa Tundu Lissu limezua hofu kubwa sit u kwa taifa, bali bara zima la Afrika na Jumuiya ya Kimataifa,” alisema Mbowe.
Alisema baada ya kupotea kwa Saanane, alimuomba Waziri Mkuu aruhusu aombe wachunguzi huru kutoka nje, lakini serikali inaonekana inakigugumizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment