Friday, 10 November 2017
Dr. Slaa Aulamba Canada, kulipwa dola 10 kwa saa katika mgahawa mmoja tu, huku akifanya kazi sehemu tatu
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Dk Willibrod Silaa (69) , ameajiliwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika.
Dk. Silaa kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1,mwaka 2015.
Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo-Supermarket.
Supermarket ya Costco anayofanya kazi DK. Slaa akihuduma kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa dola za Marekani 10 (zaidi y a sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.
Akizungumza jana kwa simu katika mahojiano maalumu, DK. Slaa alisema kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.
“Niko, ninafuatilia matukio Mutukula (ziara ya Rais DK. John Magufuli jana). Siku zote nimesema ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu. Canada ili uishi vinzuri, unahitaji kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne. Hayo nimeweka wazi, sijui jambo jipya kama mtu alikuwa hafuatilii.
“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Comunication. Costco ninakofanya kazi ina members (Wanachama) 10,000. Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema DK. Slaa.
Mbali na hilo, alisema pia anafanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na ushauri (Consultancy).
Alisema kila mara amekuwa akiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mitandao wala propaganda.
“Kanada ni kazi, Profesa wa chuo Kikuu anafanya kazi Uber, sijui kama Uber inafahamika Tanzania, ni dereva Taxi kwa kutumia gari lake binafsi. Ofisa wa serikali usiku anaosha vyombo hotelini.
“Ndio maana familia ina magari mawili au zaidi, TV, Nyumba ya kisasa, chakula chakula cha kisasa, Wanatekeleza sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa matendo. Nadhani nimekupa taarifa za kutosha ikiwa ni pamoja na kujibu Propaganda kuwa nilihongwa mabilioni.
“Niwahakikishie tena, wakati wa kusoma nilikuwa na Scholarship, tangu niaze kazi ninaishi kwa jasho la mikono yangu. Mke wangu yeye ameingia Chuo Kikuu cha York baada ya Dploma yake nab ado anapata Scholarship.
“Ndio maana tunauwezo wa kuwa na magari mawili aina ya Jeep na Dodge, ukifanya kazi utaishi vinzuri. Hii ni pamoja na kugalamiwa bima ya afya (Helth Insurance), watoto kusomeshwa na serikali ya Canada,” alisema DK. Slaa.
Mei mwaka huu, DK. Slaa, alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment