SPIKA wa Bunge la Tanzania Job Ndugai
amesema mafunzo kwa wabunge ili waweze kusoma vyema taarifa za Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
yanahitajika na wataendelea kuyatoa ili kuwawezesha wabunge kuwa na tafsiri
sahihi ya taarifa hizo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka
jimboni kwake, Spika Ndugai alisema kwamba wabunge wengi wanahitaji mafunzo
hayo kwa kuwa hawa usuli wa hesabu.
Alisema zaidi ya asilimia 70 ya
wabunge ni wapya kwa hiyo suala la mafunzo ni la lazima na tayari walishawafanyia
mafunzo kwa kuwa mafunzo hayo hutolewa kwa kila bunge.
Juzi wakati wa mafunzo ya wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ambapo mada kuu ilikuwa
uhusiano kati ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), PAC na LAAC katika kuimarisha uwajibikaji
sekta ya umma.
Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali Athuman Mbuttuka alisema kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wabunge
kuelewa kilichoandikwa kwenye ripoti ya CAG
kutokana na lugha inayotumika kuhusisha maneno ya kitaalamu.
Kutokana na changamoto hizo alitaka
mafunzo kuendelea kutolewa ili wabunge waweze kufuatilia ripoti ya kuwajibisha
serikali kwa kadiri inavyotakiwa na wala si kutumia kwa ushabiki wa kisiasa.
“Wakati mwingine Kamati za Bunge hutumia ripoti ya CAG
katika kujijenga kisiasa badala ya kuimarisha uwajibikaji,” alisema Naibu CAG huyo.
Ndugai alisema hata hivyo pamoja na
kuwafunza wabunge hao miaka mitano ikiisha wengi hubadilika na hivyo kamati
nazo hubadilika ingawa uhalisia wa taarifa hubaki ili wajumbe wapya waweze
kuendelea pale walipoachia wenzao.
Akizungumzia hoja za mabadiliko ya
mara kwa mara, Spika Ndugai alisema mabadiliko katika kamati hizo zanye wajumbe
30 hufanyika kwa mujibu wa kanuni na kwa maoni yake yeye hazijabadilishwa mara
kwa mara.
“Inapotakiwa kubadilisha wajumbe
kutokana na sababu za kimsingi hufanyika lakini kanuni zinataka wajumbe wake
miaka miwili na mara nyingi kamati hizo hutakiwa kumaliza miaka mitano. “Lakini
wakati mwingine hutokea ulazima, unapoambiwa mjumbe mmoja anapita hapa na pale
kinyume cha utaratibu hapa unatakiwa kubadili ...” alisema Spika Ndugai.
Katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa
Kamati ya LAAC, Abdalah Chikota alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa
akibadilisha kamati kila baada ya miaka miwili lakini kwa mapendekezo
yaliyofanywa na Bunge la Afrika Mashariki angalau wajumbe wa kamati wawe hata
kwa miaka mitano kwani watakuwa na uwezo mpana wa kuhoji.
Spika Ndugai katika mazungumzo yake
alisisitiza kwamba hakuna mabadiliko ya kamati na yakiyokea ni yale madogo
ambayo hayana athari.
No comments:
Post a Comment