BUNGE limetangaza kuwa, uchaguzi
mdogo wa kupata wawakilishi wawili wa nafasi ya ubunge kwa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA) kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sasa
utafanyika Mei 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Bunge, mjini hapa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa
Bunge ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi huo, Dk Thomas Kashilillah, uteuzi wa
wagombea utafanyika Mei 3. Watakaopigiwa kura na kuchaguliwa katika uchaguzi
huo wataungana na wengine saba, sita wakiwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
mmoja kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao walishinda katika uchaguzi wa
Aprili 4, mwaka huu.
Siku hiyo, Chadema licha ya kuweka
wagombea wao Lawrence Masha na Ezekiah Wenje, kura zao hazikutosha hivyo kukosa
sifa za kuchaguliwa. Walioshinda kwa upande wa CCM ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko,
Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe, Alhaji Adam Kimbisa
wakati kutoka CUF ni Ha
No comments:
Post a Comment